
ZAIDI ya shilingi milioni tatu zimetumika kununua betri jingine la kuongozea taa za barabarani lililoibwa katika Barabara ya Isevya wilayaniTabora mjini mkoani Tabora, mkoa unaoongozwa na Mkuu wa Mkoa ‘machachari’ Aggrey Mwanri.
Hasara hiyo imechukuliwa na wakazi wengi wa hapa kama hatua ya kumchokoza kiongozi huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele kupambana na watu wanaotaka kukwamisha maendeleo mkoani humo.
Tukio hilo lilifichuliwa na Mkuu wa Kitengo cha Barabara wa TANROADS mkoani humo, Raphael Mlimaji, aliyesema kwamba wizi wa betri hiyo umesababisha kusimama kutumika kwa taa za kuongozea magari katika eneo husika, hali ambayo imesababisha ongezeko la ajali za barabarani.