
UKATILI! Kitoto kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku moja kimetupwa chooni kwenye choo cha wasichana katika Shule ya Sekondari Kazima iliyopo Manispaa ya Tabora na kusababisha taharuki kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Akizungumza na vyombo vya habari katika eneoa la shule hiyo mara baada ya kuvunja choo hicho, Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Tabora, Bi. Violet Machechu, amekemea tabia ya watu wanaofanya vitendo vya kikatili mkoani humo.