×

Manara amvaa Zahera

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara

KUFUATIA Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kumuhusisha Mwenyekiti Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ na ishu ya kuihujumu Yanga kwa kumtumia meneja wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameshindwa kujizuia.

 

Hivi karibuni, Zahera aliliambia Championi lililotoka juzi Jumatano sababu za kumtimua Cannavaro ndani ya timu hiyo ni kutokana na kuihujumu timu hiyo ikiwemo kwenda ofisini kwa Mo Dewji.

 

Hata hivyo, imebainika kuwa, Mo Dewji hajakutana na Cannavaro kama Zahera alivyosema. Kutokana na hali hiyo, Manara amesema: “Kwa hili Zahera hatutakubali! Lazima uthibitishe kwamba mwenyekiti wetu wa Bodi ya Wakurugenzi alishiriki kuwahujumu kwenye mchezo wetu na nyie.

“Lazma ujue MO ni mtu mwenye heshima kubwa katika jamii, Simba haitakaa kimya, halafu unamtaja Cannavaro ili umdhalilishe, yeye ndiye nahodha bora wa muda wote Yanga, kafanya mambo makubwa.

 

“Tumekuvumilia sasa imetosha, huwezi kila siku ukaituhumu klabu yetu halafu tukukalie kimya! Sasa utajua ukubwa wa Simba. Kesi hii nimeinunua kama Mkuu wa Habari wa Simba! Nikirudi nina wewe, ulete uthibitisho kwa TFF au kwenye vyombo vya dola!”

 

Naye Zahera akajibu kwa kusema: “Manara anasema mambo mengi ya hovyo, sasa sijui ni kwa sababu gani atanishtaki kufuatana na mambo ya Cannavaro. “Anadhani anajua sheria kushinda watu wote duniani, anajidanganya. Anatakiwa ajue nimesema vile kwa sababu gani, akipata jibu hatarudia kusema alivyosema.”

STORI NA MUSA MATEJA, GPL

 

MANARA VS ZAHERA – MANARA Amlipua Tena Zahera Kocha Hana Taaluma