×

Baba D Afunguka Kufanya Kolabo na Diamond

 

BABA wa msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, mzee Abdul Juma leo ametembelea ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam,  kwenye vitengo vya Magazeti Pendwa, Global TV Online na Radio Global Online kushuhudia shughuli mbalimbali ambapo amesema atajadili na mwanaye ili aweze kufanya naye kolabo.

 

Akizungumza katika mahojiano na Global Radio, amesema: “Nitaongea na mwanangu, jambo hilo halina matatizo, kwani  kuku ni wako huwezi ukakaa nje ukampiga kwa manati,” alisema msanii huyo ambaye sasa anatamba na wimbo wa  Dudu La Yuyu.

 

Mzee Abdul Juma akiwa na mtangazaji wa Global TV, Catherine Kahabi,  alipotembelea ofisi za Global Group.
…Akiwa katika ofisi za Radio Global Online.
…Akiwa na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kushoto), Mhariri wa Championi Jumatano, Philip Nkini (wa nne kushoto) na Mhariri wa Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula.
…Akibadilishana tabasamu na Saleh Ally.

EXCLUSIVE: ‘BABA D’ ANAONGEA NA DIAMOND AFANYE NAE KOLABO |+255 GLOBAL RADIO