×

Magufuli Amlilia Mengi: ‘Nitamkumbuka kwa Mchango Wake’

RAIS John Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia na wafanyakazi wa makampuni ya IPP kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wake, Dkt. Reginald Mengi,  ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 2, 2019 akiwa Dubai katika Falme za Kiarabu (UAE).

 

“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu na maono yake yaliyopo katika kitabu chake cha ‘I Can, I Must, I Will’. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabishara,” ameandika Rais Magufuli.

 

Mengi alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro, na amefariki ikiwa ni miezi sita tangu kufariki kwa aliyekuwa mke wake, Mercy Mengi.

 

TAZAMA VIDEO YA TAARIFA HIYO YA MSIBA