×

YANGA KUANDIKA HISTORIA MPYA LEO, ZOEZI LA UCHAGUZI LAPAMBA MOTO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga, George Huruma Mkuchika akiongea na wanachama wa Yanga leo katika ukumbi wa bwalo la Polisi  jijini Dar es Salaam.

YANGA Leo Mei 5 wanaandika historia mpya kwa kuchagua viongozi wapya ambao wataiongoza timu hiyo kwa muda wa miaka minne.

Wanachama wa Yanga wakimsikiliza George Huruma Mkuchika.

Leo zoezi hilo linafanyika katika ukumbi wa bwalo la Polisi ambapo wagombea kwa nafasi zote walipata fursa ya kuzungumza sera zao na wanachama kupata fursa ya kuuliza maswali.

Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti Dr Jonas Tiboroha.

Nafasi ambazo zinagombewa ni ngazi tatu ya kwanza ni ngazi ya Mwenyekiti, ngazi ya pili ni ya Makamu Mwenyekiti na ngazi ya tatu ni ya Ujumbe wa Kamati Tendaji ndani ya Yanga.

Mgombea wa Nafasi ya mwenyekiti Dr Mshindo Msola.

Zoezi ambalo linaendelea kwa sasa ni upigaji kura ambapo matokeo yanatarajiwa kutangazwa saa 12:00 Jioni ya leo.

Mgombea pekee mwanamama katika nafasi ya makamu mwenyekiti Mhe mbunge Janeth Mbene.