Taswira ilivyoonekana eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam leo asubuhi kutokana na maji kujaa katika Barabara ya Morogoro kufuatia mvua kubwa zinazonyesha nchini tangu mwishoni mwa juma lililopita, hali ambayo ilisababisha usafiri wa magari kati ya Kariakoo na Magomeni kutokuwepo.Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipita kwa tabu eneo hilo. Hali ilivyokuwa eneo hilo.Baadhi ya wananchi wakitumia usafiri wa baiskeli za miguu mitatu maarufu kama ‘Guta’ ili kuvuka eneo hilo.
Sura nyingine ya mtafaruku huo. Waendesha bodaboda wa Magomeni Mapipa waliokuwa wakisubiri kuwasafirisha watu waliokuwa wakitoka katika sehemu iliyojaa maji.
WAKATI mvua zikiendelea kunyesha mkoani Dar es Salaam na kwengine, eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, katika Barabara ya Morogoro, lilifungwa kwa muda katika usafiri wa magari utokana na daraja sehemu hiyo kufurika na kufunikwa na maji .
Hali hiyo iliwanufaisha waendesha baiskeli za matairi matatu maarufu kama ‘guta’, walikuwa wakiwavusha wananchi katika eneo hilo kwa kuwatoza sh. 500 katika kati ya Karikaoo-Fire na Magomeni Mapipa.