×

Carol Ndosi: Tulitamani Rais Mwanamke, Sasa Tunasubiri Kuona – Video

MDAU wa Masuala ya Maendeleo na Usawa wa Kijinsia, Carol Ndosi amesaema ni hatua kubwa kwa Tanzania kama Taifa kuwa mwanamke ambaye ni Rais (Samia Suluhu Hassan), kwani wananchi walikuwa wakihitaji iwe hivyo, kwa hiyo tumefika wakati huu tusubiri kuona matokeo ya uongozi wa rais wetu.

 

Ndosi amesema hayo wakati akizungumza na +255 Global Radio; “Si kwamba vijana hawapo ‘serious’ tatizo wanakabiliwa na changamoto nyingi za kujipatia mahitaji yao ya kila siku. Unamwambia mtu hayupo ‘serious’ kwenye muktadha upi? Mfano mimi, juzi kuna mtu ameniambia siwezi kupata uteuzi kwa sababu nina rasta chafu.

 

“Kwa takribani miaka 8 sijaona jitihada za maksudi kwa ajili ya kuwakwamua vijana ukiacha mpango wa serikali kwa halmashauri kutenga 4% ya mapato kwa ajili ya mikopo ya wanawake na 4% kwa wenye ulemavu, pia Baraza la Uwezeshaji lakini silaumu Serikali.

 

Tunahitaji vijana kwenye nyadhifa mbalimbali za uongozi. Hata vyama vitoe nafasi kwa vijana hawa. Mimi si mwanasiasa wala sina kadi ya chama chochote cha siasa lakini niipongeze CCM kwa kuwapa nafasi vijana kama Shaka Hamdu (Katibu Mwenezi CCM) kwenye nafasi kubwa.

“Tunao wanawake wengi sana wenye uwezo wa kuongoza, tatizo ni namna ya kuwatambua, hatuna mfumo mzuri wa kuwatambua. Mimi ninayo initiative ambayo huwa tunawatambua wanawake 100 kila mwaka katika nyanja tofauti.

 

“Rais wangu mpendwa ninachoona sipendi ambavyo anajitetea, hahitaji kuwakumbusha watu kwamba aliyesimama hapa ni mwanamke, yani tayari ameshafika pale apige kazi. Nimependezwa na kauli yake ya kwamba atateua wasaidizi wake kulingana na uwezo wa mtu,” amesema Carol Ndosi.

 

Leave a Comment