
KONGAMANO la Victory Campus Night 2019 limefanyika usiku wa leo Mei 17, 2019 katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini.

Kongamano hilo pia limewakutanisha watu wa rika mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini na serikali ambao walijumuika na wanafunzi wa vyuo kumsifu Mungu.

Akizungumza wakati wa Kongamano hilo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, amewapa nasaha vijana hao na kusema; “Unatakiwa kujitambua wewe ni nani, unapaswa kumuomba Mungu akuondolee uoga akupe roho ya upendo, nguvu na akili na maarifa usishindwe na jambo lolote kwa uwezo wake.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo amesema; “Kila kitu kinaongea, jambo unalotakiwa kulifahamu ni kwamba ukishatoka gerezani umekuwa huru, kama unataka maisha yako yabadilike, vua gwanda na mara moja utaona mabadiliko katika maisha yako.”

Mwingine aliyepata fursa ya kuzungumza na vijana hao ni mtangazaji wa Clouds Media, Sam Sasali, ambaye amewaasa vijana kuokoka bila kujali vyeo walivyo navyo, pesa wala nyadhifa kwani kila kitu kinatoka kwa Mungu.



PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS