×

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea Ajiuzulu

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea, Peter O’Neill

Waziri Mkuu wa Papua New Guinea, Peter O’Neill amejiuzulu baada ya wiki kadhaa za kutofautiana na chama tawala.

Katika mkutano na waandishi wa habari, O’Neill amesema mabadiliko ya kisiasa Bungeni yameonesha uhitaji wa kiongozi mpya.

 

Siku ya Ijumaa Wapinzani wake walidai kuwa waneshapata idadi ya kutosha Bungeni ili kumtoa kutokana na kutoridhishwa na uongozi wake hususani jinsi alivyoshughulikia mradi wa thamani kubwa wa gesi ambao wanadai ni hasara kwa nchi.

 

Awali, O’Neill alifanikiwa kushawishi kuahirishwa kwa Bunge kwa wiki tatu ili asipigiwe kura ya kutolewa na kusema kuwa taarifa kuwa uchumi unashuka na hali ngumu ya maisha ni za uongo.

Kwa sasa Sir Julius Chan atachukua nafasi hiyo iliyoshikiliwa na O’Neill kwa miaka saba.