×

DSTV WAIPA TANO ZA KUTOSHA GLOBAL GROUP

Ofisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa  akisani kitabu cha wageni katika ofisi ya Global Group leo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Ofisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa,  leo Juni 4, 2019 ametembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam akiwa na watangazaji watakaotangaza michuano ya mashindano ya Mataifa ya Afrika 2019 ‘AFCON’ nchini Misri kwa Lugha ya Kiswahili kupitia SuperSport, Salama Jabir na Ibrahim Masoud ‘Maestro’.

Baada ya kutembezwa katika idara mbalimbali zikiwa ni pamoja na kitengo cha uzalishaji Magazeti Pendwa, magazeti ya Championi na Sport Xtra, Global TV Online, na kitengo cha Teknolojia na Mawasiliano (IT) wamesema kwamba inafanya kazi katika kiwango cha hali ya juu.

Mtangazaji mpya wa Super Spoti kwa michuano ya Afcon 2019, Salama Jabir
Mtangazaji wa vipindi vya Michezo, Ibrahim Masoud ‘Maestro’.
Meneja wa Global Group, Abdallah Mrisho (kushoto) akiongea na wageni kutoka DSTV wakiongozwa na Ofisa Masoko wa Multchoice Tanzania, Shumbana Walwa (wa pili kutoka kushoto), Maestro (wa pili kutoka kulia) na Meneja wa +255 Global Radio, Borry Mbaraka (kulia).
Mhariri Mtendaji wa Global Group, Saleh Ally (kulia) akisalimiana na Shumbana Walwa.
…Saleh akiwa katika picha ya pamoja na Ibrahim Masoud ‘Maestro’ (kulia) na Salama Jabir.
Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Samson Mfalira (kulia) akisalimana na Maestro.
Mhariri wa Gazeti la Ijuma, Sifael Paul (kulia) akisalimiana na Maestro.
…Wakiondoka katika ofisi za Global Group.
…Wakiwa katika picha ya pamoja.

Picha na Sweetbert Lukonge