×

BETIKA NA IDD EL FITRI NDANI YA GOBA , MAKONGO JUU


IKIWA leo Jumatano Waislamu duniani wakisherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri, kama kawaida Gazeti la Betika halikuwa nyuma katika kuwafikia wasomaji wake.

Betika ambalo huingia sokoni kila Jumatano, hii ni wiki ya 17 ambapo bado umaarufu wake umekuwa ukipaa siku hadi siku hadi kuzua gumzo.

Gazeti hilo ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 ambapo lina kurasa 20 za rangi.

Ndani yake kuna makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya bila ya kusahau maujanja ya kubeti.

 

Timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, leo imetembelea maeneo ya Goba na Makongo Juu jijini Dar es Salaam na kukutana na baadhi ya wasomaji ambao wameendelea kulimwagia sifa kemkem gazeti hilo.

Mmoja wa wasomaji hao aliyejitambulisha kwa jina la Masoud Issa, alisema: “Mimi nimekuwa msomaji mkubwa wa gazeti hili, kiukweli sitaacha kulisoma kutokana na maujanja ninayoyapata humu ndani.

“Katika vitu ambavyo Global mmeweza kutufurahisha zaidi wasomaji wenu, ni ujio wa hili gazeti kwani hivi sasa wazee wa kubeti tunapata urahisi katika kubeti.”

 

Kwa upande wa msomaji mwingine, Innocent John, alisema Gazeti la Betika linawahabarisha wananchi juu ya masuala ya michezo ya timu mbalimbali za soka.

“Gazeti hili linarahisisha mambo kwani kwa wale watu wa kubeti hivi sasa hawana haja ya kwenda kwenye zile sehemu maalum zilizowekwa za kubetia, badala yake ukiwa na gazeti lako popote pale unamaliza kazi yako,” alisema John.