
KAMPUNI ya Bia Nchini kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Primium Lager jana imegawabiya bure kwa mashabi na wapenzi wa Soka kwa kujipongeza watanzania kwa hatua tuliyofikia.
Zoezi la kugawa bia bure lilifanyika katika Bar mbalimbali jijini Dar es Salaam wakati wa kuhitimisha kampeni ya Friji ya Ushindi iliyokuwa ikiendelea jijini Dar as Salaam ambayo ilikuwa Watanzania tukishinda Friji ya Ushindi inafunguliwa na kugawa bia bure kwa wanywaji wa bia ya Kilimanjaro Primium Lager
.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Primium Lager, Pamela Kikuli alisema lengo la Kampeni hii ilikuwa ni kuongeza hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa Soka kama unavyofahamu Kampuni ya Tbl ni mdau mkubwa katika soka hivyo iliona ni muhimu katika kipindi kama hiki kuwa karibu na mashabiki na wadau wasoka kufurahi pamoja.
Kikuli alisema TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro wakao tayari kutoa hamasa kwa Watanzania wadau wa soka kuungana nao kila Tanzania inavyofanya vizuri kwenye soka.