×

NBC yangara maonesho ya Sabasaba, yatwaa tuzo

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan, akikabidhi kikombe cha mshindi wa kwanza katika Kitengo cha Taasisi za Fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za fedha.
…Samia Suluhu  (kushoto) akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kabla hajatembelea banda la benki hiyo. Kulia ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe.
... Samia Suluhu  (katikati) akisalimiana na baadhi ya watendaji wa NBC wakati aliporembelea  banda la benki hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba. 
..Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia), akisikiliza maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa na mmoja wa wajasiriamali. 
… akisikiliza maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na mmoja wa wajasiriamali wakati akitembelea banda la Benki  ya   NBC.  Kulia kwake ni, Theobald Sabi na kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent  Bashungwa.