×

Chongolo Atangaza Neema Kwa Walimu Watakaokubali Kwenda Kufundisha Vijijini

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ametangaza neema kwa walimu watakaokubali kwenda kufanya kazi vijijini kwa kuwa serikali inaendelea kuboresha mazingira bora ya ufundishaji kama alivyoomba Diwani wa Kata ya Magara, Mwanajacob Mwinisuri ambapo alidai kuwa katika eneo lake la utawala kuna upungufu mkubwa wa walimu.

Chongolo amesema maelekezo aliyatoa awali kwa Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa (OR) Tamisemi kuwahamishia maeneo ya vijijini, ambapo amesema amepata taarifa kuwa wapo katika mchakato wa kuwahamisha walimu kutoka maeneo ambayo walimu idadi yao imekuwa kubwa.

 

Pamoja na hilo, pia ametoa maelekezo kwa serikali kuongeza madarasa kwenye shule za msingi kote nchini kwa kuwa wazazi wengi kwa kipindi cha miaka mitano watoto wengi wamekuwa wakianzishwa masomo hali iliyoplekea upungufu kwa shule wa madarasa.

Leave a Comment