
WATU wanne wamefariki, akiwemo ofisa mfawidhi wa ulinzi wa raslimali za uvuvi kanda ya Ukerewe, Ibrahim Njalali na askari polisi mmoja kujeruhiwa katika tukio la mapigano baina ya wananchi na kikosi cha doria cha kuzuia uvuvi haramu katika kisiwa cha Siza karibu na kisiwa kikubwa cha Ghana wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
Tukio hilo limetokea leo baada ya wananchi kutofautiana na kikosi hicho na hivyo kuibuka mzozo uliosababisha kadhia hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amethibitisha tukio hilo na kusema mamlaka husika zipo katika hatua za uchunguzi.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza inatarajia kuondoka kesho jijini Mwanza kuelekea eneo la tukio.
CHANZO: ITV