×

Aishi Manula Kuikosa Kenya leo, Kikosi Kipo Hapa

NYOTA wawili wa kikosi cha timu ya taifa, ‘Taifa Stars’, Kipa Aishi Manula na beki David Mwantika wataukosa mchezo wa kwanza kufuzu fainali za CHAN, dhidi ya Kenya, ‘Harambee Stars’, utakaochezwa leo Jumapili saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa.

Kukosekana kwa Manula kunampa nafasi kubwa kwa nahodha msaidizi wa timu hiyo, Juma Kaseja kuanza pambano hilo la leo la kuwania Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani zitakazochezwa mwakani nchini Cameroon.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania Cliford Ndimbo, inaeleza kuwa wachezaji hao hawatakuwa katika mchezo wa leo jioni dhidi ya Kenya kutokana na majeraha ambayo wameyapata.

“Taarifa zaidi za kitabibu zitafata kueleza aina ya majeraha ambayo waliyapata wachezaji hao mpaka kushindwa kuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kitacheza dhidi ya Kenya,” alisema Ndimbo.

JESHI zima la timu ya Taifa leo uwanja wa Taifa dhidi ya Kenya

1.Juma Kaseja
2.Paul Godfery
3,Gadiel Michael
4.Erasto Nyoni
5.Kelvin Yondan
6.Jonas Mkude
7.Hassan Dilunga
8.Salum Abobakar
9.John Bocco
10.Ayubu Lyanga
11.Idd Seman

Akiba

12.Metacha Mnata
13.Frank Domayo
14.Kelvin John
15.Ibrahim Ajib
16.Abdul Aziz
17.Idd Majaliwa
18.Salim Aiyee