
Klabu ya Yanga imemalizana na aliyekuwa mcheza wao Gael Bigirimana raia wa Burundi ambae aliwafungulia kesi Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) baada ya klabu ya hiyo kushindwa kumlipa mchezaji pindi walipovunja mkataba na mchezaji huyo.
Klabu ya Yanga ilifungiwa usajili na FIFA baada ya kushindwa kumlipa mchezaji huyo ndani ya siku 45 ambao ulikuwa uamuzi wa FIFA baada ya Bigirimana kushinda kesi yake dhidi ya Yanga
Yanga imeondolewa adhabu hiyo ya kutosajili baada ya kumlipa mchezaji huyo kiasi cha pesa alichokuwa akiwadai.
