×

Mzungu Simba ampa Kapombe dk 60

Patrick Aussems.

KOCHA mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameamua kumpa mbinu maalum beki wake Shomary Kapombe ya kurejea katika uwezo wake kwa kumchezesha dakika 60 tu katika mechi zao.

 

Kapombe kwa muda mrefu hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kutokana na majeraha ambapo alirejea hivi karibuni na kuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wapo kambini nchini Afrika Kusini. Beki huyo akiwa na Simba nchini Afrika Kusini tayari amecheza mechi tatu dhidi ya Orbret TVET, Platinum Stars na jana dhidi ya Township Rollers.

Beki huyo amesema kwa sasa anaendelea vizuri ambapo ili kurejea kwenye kiwango chake ambapo mwanzoni alikuwa akipewa dakika 30 pekee za kucheza kabla ya kuongezewa
kwa sasa na kufika 60.

 

“Naendelea kujiandaa nikiwa nafanya mazoezi ninayopewa ili kuwa sawa. Kocha alinipa dakika 30 kisha baadae akaniongezea 60 na muda siyo mrefu ninaamini nitamaliza 90, Mungu atanisaidia niwe fiti na ninashukuru kwa hapa nilipofika, maandalizi yako vizuri na kambi iko vizuri, kikubwa tunaendelea kufanya mazoezi kwa nguvu,” alisema Kapombe, ambaye ni mkazi wa Temeke.