HUJAFA HUJAUMBIKA! Kijana Hamad anayeishi Majumba-Sita, Ukonga, jijini Dar es Salaam amewaomba Watanzania kumsadia ili aweze kwenda India kupatiwa matibabu kutokana na tatizo linalomsumbua lililosababisha maisha yake ya sasa kuwa ni ya kutumia mashine ya oksijeni tu na endapo umeme ukikatika ndani ya siku tatu tu, basi anapoteza maisha. Kwa siku anatumia umeme wa Tsh. 50,000/-.
Global TV imemtembelea Hamad nyumbani kwake na kuzungumzia naye kuhusiana na hali yake na nini hasa kilimkuta hadi kufikia hatua hiyo.