×

Bocco Nje ya Uwanja Wiki Tatu

BAADA ya kufanyiwa vipimo na kugundulika majeraha yake, mshambuliaji tegemeo wa Simba atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu akiuguza majeraha ya goti.

 

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam, alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo huko Beira, Msumbiji.

 

Akizungumza na Spoti Xtra ambalo hutoka kila Alhamisi na Jumapili, Aussems alisema Bocco amefanyiwa vipimo kwenye Hospitali ya Muhimbili, Dar.

 

Aliongeza kuwa kukosekana kwa Bocco ni pengo kubwa katika kikosi chake, licha ya kuwepo wengine kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao.

“Kabla ya mchezo wetu na UD Songo nilikuwa nimeingia hofu ya kutofanya vizuri kutokana na kumkosa Bocco. “Kukosekana kwake nililazimika kubadili mfumo nikimtumia mshambuliaji mmoja pekee ambaye ni Kagere, hivyo lilikuwa tatizo kwangu kiufundi,” alisema kocha huyo mashabiki wanadhani angempa nafasi Tshabalala kwenye kikosi cha kwanza badala ya Gadiel Michael.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaa