×

DC Kigamboni Sarah Msafiri Ataja Mikakati Yake | +255 Global Radio

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa pili kulia), akisalimiana na Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, wakati akipokelewa katika ofisi za Global Group zilizoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Mhariri Mtendaji wa magazeti la Global Publishers, Saleh Ally, na kushoto ni Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli.

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri,  amesema wilaya yake imejipanga kuhakikisha inatokomeza uhalifu na unyanyasaji wa kijinsia ambao umekuwa ukijitokeza katika maeneo mbalimbali ya Kigamboni ikiwemo tukio la mwanamke Naomi aliyeuawa na anayedaiwa kuwa mumewe, kisha kuchomwa moto kwa magunia mawili ya mkaa.

…Akisaini kwenye kitabu cha wageni.

Ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano ya +255 Global Radio alipotembelea ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kutoa taarifa mapema wanapoona matukio kama hayo au viashiria vya unyanyasaji kama huo.

…Akikabidhiwa gazeti la Ijumaa na Mhariri Paul Sifael; moja ya magazeti ambayo huchapishwa na Global Publishers.

…Akikabidhiwa gazeti la Championi Jumamosi na  Mhariri Lucy Mgina.

…Akiwa ndani ya studio za +255 Global Radio.

…Akiwa na Saleh Ally, Abdallah Mrisho na Mkuu wa Global Radio, Borry Mbaraka.

Aidha,  amewataka wananchi kuyaendeleza maeneo waliyopewa wilayani humo kwani wasipoyaendeleza ndani ya miaka mitatu yatataifishwa na kuwa mali ya serikali.

…Akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Global Group, Eric Shigongo.

Mkuu huyo wa wilaya ameonyeshwa vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya ofisi za Global Group zikiwemo za kitengo cha Global Publishers kinachozalisha magazeti, kitengo cha Global TV Online na mwisho akamalizia kwa mahojiano na kitengo cha Global Radio.