MBUNGE wa Mbeya mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Joseph Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’ leo tarehe 31, Agosti, 2019, amefunga pingu za maisha na mchumba wake Happiness Msonga.
Ndoa hiyo ambayo ilitangazwa siku kadhaa zilizopita imefungwa leo katika Kanisa Katoliki la Ruanda lililopo jijini Mbeya.
Baadhi ya wabunge wameungana naye katika siku hiyo muhimu akiwemo swahiba wake Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haule amepost picha akiwa kanisani kushuhudia tukio hilo muhimu.
Picha zaidi na video za tukio hili tutakuwekea hapa hapa