×

Taifa Stars Yaibana Burundi, Msuva Afanya Kweli

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeibana Timu ya Taifa ya Burundi baada ya kulazimisha sare ya ba0 1-1, mechi iliyochezwa jioni ya leoJumatano, Septemba 4, 2019, katika Uwanja wa Prince Louis Rwagasore.

Katika mechi hiyo ya hatua ya awali kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia, Stars walianza kwa kushambulia huku wakikosa nafasi nyingi.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Stars walikuwa wakimiliki mpira vizuri na kulisakama mara kadhaa lango la Burundi.

 

Lakini kipindi cha pili hali ilikuwa tofauti kidogo baada ya Burundi kulisakama lango la Stars wakitafuta bao kwa udi na uvumba, kosa kosa za hapa na pale, hadi dakika ya 80 ambapo mshambuliaji Cedric Amisi aliiandikia Burundi bao la kuongoza baada ya kuachia shuti kali ndani ya 18.

 

Dakika 5 baadaye, Simon Msuva alinyanyua furaha ya Watanzania baada ya kuisawadhishia Taifa Stars kwa mpira wa counter attack ambapo mabeki wa Burundi pamoja na kipa wao walijichanganya na kumpa upenyo wa kutumbukiza wavuni.