
NDEGE ya Air Tanzania Airbus A220-300 iliyokuwa ikishikiliwa Afrika Kusini imekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk. Damas Ndumbaro, leo Septemba 4, 2019, baada ya Mahakama Kuu ya Gauteng chini ya Jaji Lamont, kutupilia mbali tena ombi jingine la Steyn aliyetaka, pamoja na uamuzi wa awali leo, ndege iendelee kushikiliwa.
Alasiri hii, jaji huyo amesema mahakama hiyo haina uwezo (jurisdiction) wa kusikikiza kesi hiyo.


Awali, mahakama hiyo ilitoa hukumu na kuamuru ndege hiyo iliyokuwa ikishikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi.

“…Hoja zote zilizotolewa na mawakili wetu zimeshinda, na tumeshinda kesi hiyo, na imeamriwa ndege hiyo ya Air Tanzania iweze kuondoka,” alisema Dkt. Ndumbaro.

UPDATES: Hata hivyo, muda mfupi baada ya mahakama hiyo kuamuru ndege hiyo iachiwe, mkulima aliyepeleka shauri hilo mahakamani, Hermanus Steyn, amekata rufaa kwa madai ya kutoridhishwa na hukumu hiyo. Shauri hilo linatarajiwa kuanza kusikilizwa leo Septemba 4, 2019.
