×

Mwl. Mkuu Akamatwa Baada Binti Aliyemkana Kukamatwa

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, ACP Martin Ottieno amesema tayari jana usiku wamemkamata kwa mara nyingine Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore, Jason Rwekaza (42) ambaye aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu mkazi Kigoma Septemba 16 baada ya mwanafunzi kukana ushahidi alioutoa polisi mbele ya mahakama kwamba hamfahamu aliyeshiriki naye mapenzi hadi kupata mimba.

Kamanda ACP Ottieno amesema kuna jambo lililomshawishi mwanafunzi kufikia uamuzi huo na sasa wanaandaa mashtaka dhidi ya mwalimu huyo kwa makosa yanatomkabili na muda siyo mrefu watamfikisha mahakamani.