×

Meridianbet Yagawa Mipira Kijitonyama

Meridianbet Agosti 13, 2024 wamefika eneo la Kijitonyama jijini Dar-es-salaam na kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu mbili zinazopatikana katika eneo hilo kuhakikisha wanainua michezo katika jamii.

 

Magic Fc, African Boys ni timu ambazo zimenufaika na msaada wa Meridianbet leo ambapo wamefika katika timu hizo na kugawa mipira kadhaa  kwa kila timu, Hii ni mwendelezo wa yale ambayo wamekua wakiyafanya kampuni hiyo kurudisha kwa jamii.

 

Huu umekua ni utaratibu kwa kampuni ya Meridianbet kuhakikisha wanashika mkono wale wote ambao wamekua na uhitaji, Na ndicho walichokifanya mapema leo katika eneo la Kijitonyama jijini Dar-es-salaam.

 

Bashiri michezo mbalimbali ambayo imepewa ODDS BOMBA pale Meridianbet wikiendi hii Bila kusahau kucheza michezo ya Kasino uibuke mshinde wa Mamilioni

 

Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wanatambua fika kua michezo imekua sehemu inayotoa ajira kwa vijana wengi haswa mpira wa miguu, Hivo wao kutoa msaada kwa timu hizo za mpira wa miguu imeonesha kua wanapambana kuhakikisha ajira zinapatikana kwa wingi kwa vijana kupitia michezo.

 

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka Meridianbet Nancy Ingram alipata wasaa wa kuzungumza wakati wa tukio hilo “ Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani kwa mapokezi mliyotupatia mahala hapa lakini kubwa ni kufanikisha hili ambalo tumelifanya hapa tuna matumaini tutapata wachezaji wazuri sana siku za mbeleni kupitia timu hizi”

Aidha viongozi wa timu za Magic Fc, pamoja na African Boys walifanikiwa kutoa shukrani zao za dhati kwa uongozi wa Meridianbet kwa msaada walioutoa kwao wakitoa wito kwa makampuni mengine kujitahidi kutoa misaada ili kuhakikisha wanaibua vipaji vipya kila siku.

Leave a Comment