
MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar, Kiduma Siga Mageni, ametoa maelekezo muhimu kuhusu uchaguzi huo.
Msimamizi huyo amepewa mamlaka chini ya Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi wa Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika tangazo la Serikali namba 372 la Aprili 26, 2019 katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Akizungumza na Global Publishers leo jijini Dar, Kiduma alisema uchaguzi huo utafanyika Novemba 24, mwaka baada ya zoezi la uandikishwaji wa wapiga kura litakalofanyika kuanzia Oktoba 8 hadi 14, mwaka huu.
“Natangaza kuwa uchaguzi utafanyika Novemba 24, 2019, hivyo wananchi wanatakiwa wajiandikishe ili waweze kupata fursa ya kuchagua viongozi wao watakaowaongoza.
“Vituo vya kujiandikishia vitakuwa wazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwenye mitaa 106 ya Kata 20 za Kinondoni.
“Wananchi wote wenye sifa za kupiga kura, kwa mujibu wa kanuni ya 13 mnatakiwa kujiandikisha kwenye vituo vya uandikishaji wapiga kura vilivyopangwa kila mtaa.

“Wakazi wote wenye umri wa miaka 21 au zaidi wanatakiwa kugombea nafasi ya uenyekiti wa mtaa au ujumbe wa kamati ya mtaa wanatakiwa kuchukua fomu za kugombea kwenye Ofisi za Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa kila Mtaa.
“Fomu ya maombi ya kugombea Uenyekiti wa Mtaa au Ujumbe wa Kamati ya Mtaa zitatolewa kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 5, 2019.
“Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni Novemba 5, 2019 saa 10:00 jioni kwenye ofisi ya msimamzi msaidizi wa uchaguzi wa kila mtaa na siku ya uteuzi wa wagombea itakuwa Novemba 5, 2019 saa 10:00 jioni,” alisema msimamizi huyo.
Stori: Neema Adrian, Global Publishers