Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, Angellah Kairuki, akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Kikosi cha JKT 842 Mlale wanaosimamia kiwanda cha kuchakata mahindi kinachohudumiwa na kikosi hicho wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira ya uwekezaji katika mkoa wa kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Septemba 23, 2019.
Kamanda wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akizungumza katika hafla hiyo.
Kairuki akifuatilia hotuba ya Shausi.
…Akionyeshwa mitambo ya kuchakata mahindi na kusaga unga wa sembe.
Baadhi ya mifuko ya unga wa sembe inayotengenezwa na kiwanda hicho.
…Akipata maelezo kuhusu magunia ya pumba za mahindi yaliyohifadhiwa baada ya kuchakata na kutoa unga wa sembe.
Baadhi ya vijana wa JKT wakiimba wimbo wa kumkaribisha Kairuki.
Kairuki akiteta jambo na Shausi.
…Akipokea zawadi ya unga wa sembe.
…Akizungumza na vijana wa JKT.
Sehemu ya watumishi wa serikali waliohudhuria wakati wa ziara hiyo.