×

Naibu Waziri Mkuu Kushiriki Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Agosti 28, 2024 amewasili jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika ( US-Africa Nuclear Energy Summit).

Mkutano huo wa masuala ya Nyuklia utahusisha mijadala kuhusu utayari wa Sekta ya Nishati katika kusimamia mnyororo wa thamani kwa ajili ya uendelezaji wa nyuklia pamoja na umuhimu wa kuwashirikisha wanawake na vijana katika Sekta.

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameambatana na Watendaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Nishati na Wizara ya Madini.

MBUNGE SHIGONGO AFUNGUKA ISHU ya MA-RC na MA-DC KUTUMIA SHERIA ya SAA 48 KUWAWEKA WANANCHI LOKAPU…

Leave a Comment