
Askofu Mkuu jimbo Katoriki la Dar es Salaam, baba Mwashamu, Yudatadei Ruwai’ch ameruhusiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza wakati akiruhusiwa hospitalini hapo, Ruwai’ch ameishukuru serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Magufuli kwa ushirikiano wake mkubwa wa kuhakikisha afya yake inatengamaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Respicius Boniphace amesema kuwa tiba zilizopo katika Taasisi hiyo zilizo bora ndizo zimepelekea kuokoa uhai wake na kuwataka watanzania kuendelea kuiamini Taasisi hiyo.
