×

P Mawenge Aachia Ngoma Yake Mpya ‘UNGENIAMBIA’ – Video

MSANII wa Bongo Fleva, P Mawenge (P The MC), ameachia wimbo wake mpya uitwao “UNGENIAMBIA” ambao tayari upo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na platforms za muziki duniani.

P The MC ambaye ni heat maker wa ngoma ya Mitaa Nayotoka ametangaza ngoma yake hiyo kwenye  kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 10:00 jioni kupitia +255 Global Radio.

Akipiga stori na Bongo 255, P Mawenge ameeleza mikakati yake ya kufanya ngoma na msanii mkubwa nchini Marekani ambaye wanafanana kwa majina (naye anaitwa P The MC).

“Msanii P The MC wa Marekani nilikutana naye kwenye social networks, baada ya kuona kazi zake wakati huohuo majina yetu kumbe yanafanana, tulipiga stori na baadaye akaomba kazi zangu.

“Nimeshamtumia bit zangu nne, ameshazicheki, ninasubiri mambo yake yakae sawa then tunaingia studio na kutengeneza kitu kitakachotikisa dunia,” amesema P Mawenga (P The MC).