
CHAMA cha Democrats nchini Marekani kimeanzisha uchunguzi rasmi dhidi ya rais wa nchi hiyo Donald Trump kuhusiana na madai kwamba alitaka usaidizi kutoka Ukraine ili kumuangamiza hasimu wake wa kisiasa.
Spika wa bunge la congress kutoka chama cha Democrats Nancy Pelosi amesema kuwa rais Trump lazima awajibike kutokana na madai hayo yanayo mkabili.
Kwa upande wake Rais Trump amekanusha madai hayo na amezitaja tuhuma hizo kama hila chafu dhidi yake.