×

Ramaphosa Amteua Aliyekuwa Gavana BoT

RAIS Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua Prof. Benno Ndulu kuwa miongoni mwa watu 18 wanaounda baraza la kumshauri  katika masuala ya uchumi litakaloanza kufanya kazi kuanzia Oktoba 01, 2019.

 

Baraza hilo lililotangazwa jana na Ramaphosa litakuwa na kazi  ya kuhakikisha uhusiano mzuri na uthabiti katika utekelezaji wa sera ya uchumi na kuhakikisha kuwa serikali inaweza kujibu mabadiliko ya hali ya uchumi.

 

Baraza linajumuisha viongozi wa ndani na nje ya Afrika Kusini watakaotoa mawazo ya kiuchumi, wakishauri kwa upana zaidi, kuwezesha maendeleo na utekelezaji wa sera za uchumi zinazochochea ukuaji wa umoja.

 

Pamoja na Prof. Benno Ndulu, wengine ni Prof. Mzukisi Qobo, Prof. Dani Rodrik, Prof. Mariana Mazzucato, Mamello Matikinca-Ngwenya, Dkt. Renosi Mokate, Dkt. Kenneth Creamer, Prof. Alan Hirsch, Prof. Tania Ajam, Dkt. Grové Steyn, Wandile Sihlobo, Dkt. Liberty Mncube, Prof. Fiona Tregenna, Prof. Haroon Bhorat, Ayabonga Cawe, Prof. Vusi Gumede, Dkt. Thabi Leoka na Prof. Imraan Valodia.

 

Prof. Benno Ndulu alikuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania tangu 2008 hadi 2018 baada ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Florens Luoga kushika nafasi hiyo.