
MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, amekabidhi vitanda vitano vyenye dhamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 katika kituo cha afya chaNyamisu kilichopo Kisiwa cha Kome.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vitanda hivyo, Mhe. Shigongo amewataka madaktari na wauguzi wa kituo hicho kutoa huduma kwa moyo mmoja ili kuwahudumia wananchi vizuri na kuokoa maisha yao.

Aidha, amesema kutokana na changamoto zilizopo kwenye kituo hicho amewaomba watu wengine pamoja na wana-Buchosa wanaoishi maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi kusaidia maendeleo ya Jimbo la Buchosa.
