Msanii wa muziki wa Bongo fleva Hellen George maarufu kama Ruby usiku wa kuamkia leo, Septemba 29, 2019 amedhihirisha kwamba yeye ndo malkia wa viuno kwa sasa Bongo baada ya kufanya bonge la shoo kwenye Tamasha JamaFest lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akikinukisha na msanii kutoka WCB Rayvanny, Ruby mwenye sauti nyembamba na ya kuvutia wakati anaimba, alikata mauno ile mbaya hadi wanaume wakachanganyikiwa na kuivamia steji ili waruke naye ngoma.
JamaFest ni Tamasha ambalo limehitimishwa usiku wa kuamkia leo, liliwakutanisha nchi za Afrika Mashariki kuonyesha tamaduni zao.