ALIYEKUWA kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Cornell Apson Mwang’onda (75), amefariki dunia mchana wa leo, Jumatatu, Oktoba 7, 2019 mjini Pretoria, Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Familia imethibitisha na kusema itatoa taarifa zaidi baadaye.
Apson Mwang’onda alistaafu kazi hiyo Agosti 21, mwaka 2006 kwa mujibu wa sheria.