×

Rais Magufuli Azindua Barabara ya Sumbawanga – Chala


Rais Dk. John Magufuli leo, Jumanne, Oktoba 8, 2019 anatarajia kuzindua barabara ya lami ya kilomita 76 kutoka Sumbawanga –Chala hadi Kanazi mkoani Rukwa iliyogharimu Sh. bilioni 61.

 

Tukio hilo litafanyika katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi kwenye Uwanja wa Sabasaba ambapo pia anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo.