×

JPM: Ningetaka Utajiri Ningekuwa Bilionea – Video

Rais Dkt John Magufuli, leo Oktoba 10, 2019 anaendelea na ziara yake mkoani Katavi ambapo ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujnzi wa Barabara ya lami ya Mpanda – Tabora pamoja na kuzindua kituo kipya cha mabasi kilichopewa jina la Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Kayanza Peter Pinda

 

Akizungumza na wananchi wa Mpanda mkoani humo wakati akilihutubia Taifa, Rais Magufuli amnesema haya;

 

“Nimekuwa waziri kwa miaka 20, ningekuwa na shida na utajiri si ningekuwa bilionea? Lakini kazi niliyoimba mimi ni moja tu, nchi hii niinyooshe, nimewaanyoosha mafisadi, walituchezea mno, walituibia mno. Wamedhulumu rasilimali za Watanzania.

 

“Ninanchotaka tu kuwaomba ndugu zangu chapeni kazi, mengine mtuachie serikali, nataka miaka inayokuja mtu awe anatoka hapa anakula breakfast hapa, lunch anakwenda kula Tabora, dinner anakula hapa jioni.

 

“Mkandarasi asisubiri mpaka mwisho wa mkataba ndipo amalize hii barabara, ninataka afanye kazi haraka, amalize kabla ya muda…. Hii si barabara ya Kitaifa ni ya Kimataifa. Mpanda ndipo patakuwa kitovu.”

 

“Ninatoa maagizo kwa Ofisa Elimu wa Mkoa wa Katavi, usipange walimu mjini tu, wapange na vijijini, asiyetaka kwenda kijijini aache kazi ya ualimu. Vijijini ndiko tulikozaliwa, hata madaktari, manesi na watumishi wengine wapangwe vijijini.

 

“Hatuwezi kuwa watumwa kwenye nchi yetu. Maaskari walikuwa wanakwenda kuchoma nyumba za watu, hapa Katavi niliona mama amechomewa mahindi yake tena akiwa amejifungua mapacha, nikasema hapana, ni lazima nikatumike kufungua maisha ya wanyonge.

 

“Mawaziri, wakuu wa mikoa, Ma-DC na watumishi wengine wanashida mno kwenye utawala wangu, wanachapa kazi kweli kweli. Wanatumika kama ninavyowatumikia mimi, hawalali. Watazameni hata sura zao.

 

“Mbuga ya Katavi ina umuhimu wa pekee, hata mti wa kutambikia nao upo hapa, pia Chifu amesema wamechoka kusafiri kwa ungo, inabidi kuwe na mashindano mmoja asafiri kwa ungo, kwenda Dar es Salaam, mwingine apande Ndege, tuone nani atawahi kufika.

 

“Jana nimetembelea hifadhi ya Katavi, maji yamekauka na viboko wanateseka sana. Kutokana na ukame, mionzi ya ultra violet inawaathiri viboko hao, wanachanika. Niwaagize TANAPA, kuanzia kesho mchimbe bwawa, mjaze maji mle. Mkuu wa Mkoa simasima hilo.

 

“Napendekeza mfungue bucha la nyama ya porini hapa Katavi, muuze nyama ya viboko, swala, mbogo. Vuneni kwa utaratibu angalau kwa wiki mara moja. Haiwezekani mtu uzaliwe hapa karibu na pori la Katavi mpaka ufe meno yako hayajaonja nyama ya porini.

 

“Mpanda kuna vyakula vingi vizuri, jana nimekula hapa karanga nikatamani nilalie karanga tu kila siku. Kila kitu cha hapa ni kitamu kwelikweli. Kuna wakimbizi laki 1.2 walipewa uraia tukawaambia waishi kama raia, baadhi yao wanafanya shughuli za ujambazi, huwezi mtu ukakaribishwa kwa shida ulizozitengeneza kwenu halafu ukaja ukazileta hapa.

 

“Niwaombe wakimbizi mkae kwa amani ila Burundi imeanza kuwa na mani na utulivu mkubwa, wanaoweza kurudi warudi kuendeleza nchi yao, wanaotaka kukaa wakae kwa amani hadi utaratibu mwingine utakapowekwa, msifanye ujambazi.,” amesema Magufuli.