
SHINDANO la Miss Utalii limeingia makubaliano ya kudhamini shindano la Kimataifa la Miss Utalii Tanzania 2019/2020 na hotel ya kitalii ya Jaromax Palace Hotel ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa mashindano hayo, Georgina Saulo, amesema wameingia makubaliano hayo ili kufanikisha sera ya taifa ya utalii na uungaji mkono kwa vitendo wa jitihada kubwa zinazofanywa na serikali.

“Tumeamua kuungana na hoteli hii kwa sababu ni uthibitisho wa hadhi na ubora wa hoteli hiyo na huduma zake ambazo ni za kitalii na pia shindano letu litakuwa linahusha vitu vya Kiafrika yakiwemo mavazi yatakayovaliwa na tamaduni zetu za Afrika, hivyo kulifanya shindano hilo kuwa la kimataifa likishirikisha washiriki wa ndani na nje ya nchi, na kupanua wigo wa wawekezaji, wafanyabiashara na nchi kujitangaza kimataifa kupitia shindano la washiriki kutoka nchi mbalimbali,” alisema Georgina.
Matukio katika picha:




Mandhari ya nje ya hoteli hiyo.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN