×

Alichonga Fimbo ya Nyerere, Sasa Achonga ya JPM

MCHONGA vinyago, Mzee Omary Mwariko aliyechonga kifimbo alichokuwa anakishika Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ameandaa kifimbo kingine kwa lengo la kumkabidhi Rais John Magufuli kama alama ya kumuenzi Mwalimu.

 

Mzee huyo ambaye ni mkazi wa Kilimanjaro amesema: “Ndani ya Tanzania kuna makabila mengi na kila moja lina imani yake. Mti unaotumika kutengnezea kifimbo hicho ni mti wa ki-chifu unaoitwa mkuru.

“Fimbo niliyompa Baba wa Taifa ni fimbo yenye uwezo mkubwa wa kusaidia katika mambo mbalimbali ya Tanzania katika mila, jadi na desturi. Hii anayokwenda kupewa Magufuli imeongezwa ukali zaidi ili iwaweze mafisadi na wale wanaokuwa hawaeleweki mbele zake.”

 

Aidha, amemalizia kwa kusema kuwa ana imani kabisa kwa namna atakavyoongea naye rais ataipokea fimbo hiyo, ila kwanza anataka kukutana na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ili amuunganishe aweze kuonana na Rais Magufuli.

 

CREDIT: AZAM TV