JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya JKT/JKU waliopo kwenye Makambi ya JKT/JKU wenye elimu ya kidato cha Nne, kidato cha Sita, Stashahada na Shahada.
Waombaji wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;
- Awe Mtanzania wa kuzaliwa
- Awe amehitimu mafunzo ya awali ya JKT/JKU na ana cheti cha kuhitimu mafunzo hayo katika operesheni mbalimbali.
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi 25 kwa wenye elimu ya kidato cha nne, sita na stashahada
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi 28 kwa wenye elimu ya shahada
- Awe na elimu ya kidato cha nne aliyemaliza mwaka 2017, 2018, 2019, 2020 na ufaulu wa daraja la nne alama (point) 29, 30, 31, na 32
- Awe na elimu ya kidato cha sita aliyemaliza mwaka 2017, 2018, 2019, 2020 na ufaulu wa daraja la tatu na la nne.
- Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma (academic certificates) pamoja na vyeti vya shule aliyohitimu (leaving certificates)
- Awe na picha tatu za rangi
- Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho ya taifa (NIDA).
- Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa serikali
- Awe na tabia njema iliyothibitishwa kutoka Shule aliyosoma/ Serikali ya mtaa/ Serikali ya kijiji/ Shehia na Wakuu wa makambi.
- Asiwe na kumbukumbu za uhalifu
- Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto
- Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo)
- Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi tano (5’ 5”) kwa wanaume, na futi tano inch tatu (5’3”) kwa wanawake.
- Awe hajawahi kutumia aina yoyote ya madawa ya kulevya
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Taaluma ya Polisi
- Awe hajaajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali
- Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania
- Waombaji watakaofaulu usaili ndio watakaochaguliwa.
- Waombaji wote waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) na kuziwasilisha kwa wakuu wa kambi za JKT/JKU, walipohitimu mafunzo yao wakiambatisha nakala za vyeti.
- Waombaji wenye masomo/taaluma za sayansi na Ufundi watapewa kipaumbele.
- Usaili utafanywa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa
- Mwisho wa kupokea maombi hayo ni tarehe 30/08/2021
- Waombaji wote waandike barua kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Sanduku la Posta 961 Dodoma kupitia Wakuu wa Kambi JKT/JKU.
Inasisitizwa Muombaji awe amehitimu mafunzo ya JKT/JKU na ana cheti halisi cha kuhitimu.
Imetolewa na;
Inspekta Jenerali wa Polisi
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
S.L.P 961
4 Barabara ya Posta
40483 DODOMA