JPM Azungumza na Viongozi wa AALCO, Waziri wa China
Global Publishers October 23, 2019
SHARE THIS:
RAIS John Magufuli leo Oktoba 23, 2019, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais John Magufuli akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika nchini kwa siku tano ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali, walipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam. leo Oktoba 23, 2019.
…Akiwa na Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran) na Amon Mpanju Naibu, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria (Tanzania).
…Akiagana na Prof. Mohamad Shalaldeh.…Akiagana na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.…Akiagana na Bi. Wang Liyu Naibu, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria wa China.…Akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Guo Yezhou.