×

Hamisa ampa mama’ke ndinga matata!

NANI kama mama? Najua unajibu kimyakimya kuwa hakuna! Unaambiwa mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto amemzawadia mama’ke, Shufaa Rutiginga gari matata aina ya Toyota Alphard.  Gazeti la Ijumaa lina data kama zote kwamba, mwanamama Hamisa sasa hivi mambo ni moto maana pesa zimemtembelea na maisha yake siyo ya kubahatisha.

Mapema wiki hii, Hamisa alitupia picha na vipande vya video akishuti kideo chake kipya huko visiwani Zanzibar kuonesha kwamba muziki unamlipa. Lakini nyuma ya pazia, kuna madai mengine mazito kwamba, ‘vurugu’ zote hizo anazozifanya Hamisa zinatokana na kuwa na bwana mpya anayempa maisha mjini.

Katikati ya vurugu hizo, Hamisa ametupia picha za gari hilo jipya kwenye Insta Story yake na kuweka wazi kuwa ni zawadi kwa mama yake huyo ambaye amekuwa naye katika shida na raha na kwenye milima na mabonde. Kwa upande wake, mama Hamisa alimshukuru binti yake huyo kwa kumjali. Huku akisindikizia picha za gari hilo, mama Hamisa aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram;

“Alhamdulilaah kwa kila jambo mwanangu. Allah akuongezee zaidi na zaidi ulipotoa. Allah akupe kikubwa zaidi, nakupenda sana na nakuombea siku zote.” Gari hilo Hamisa alilomnunulia mama yake linagharimu kati ya shilingi milioni 18 hadi 25 za Kibongo.