×

Yanga: Tunapindua Matokeo leo dhidi ya Pyramids, Misri

PAMOJA na maombi na juhudi za kila namna nje ya uwanja, Yanga leo inahitaji matokeo ya aina tatu tu vinginevyo maji yatazidi unga. Yanga inarudiana na Pyramids nchini Misri leo saa tatu usiku katika mechi ambayo wakishinda wanafuzu hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika.

 

Kutokana na kipigo cha mabao 2-1 walichopata jijini Mwanza, Yanga wanahitaji ushindi wa mabao 3-1 ili kufuzu. Lakini vilevile matokeo mengine mawili ambayo ni mabao 3-0 au mabao 2-0 wakiyapata yanaweza kuwabeba Yanga.

Ingawa mashabiki wameonekana kutokuwa na imani kutokana na kiwango walichokishuhudia kwenye mechi ya awali. Lakini Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amewaambia yuko Misri kupindua meza.

 

“Lengo letu ni kuona tunafanikiwa kushinda mchezo huu ili tuweze kusonga mbele, kikosi kipo vizuri, kila mchezaji anaonyesha hamasa kubwa ya ushindi pia kama uongozi tumekutana nao kwa ajili ya kuwapa hamasa na wamehamasika.

“Tumefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo, timu imefanya mazoezi katika kiwanja safi, hoteli nzuri na usafiri wa ndani unaridhisha, tunaamini mwalimu amefanyika kazi makosa yaliyojitokeza mchezo uliopita.

 

“Tumeshakamilisha suala zima la mashabiki kutokana na Watanzania wengi waishio huku kujitokeza na kutoa sapoti, pia tumepata mapokezi mazuri kutoka kwa balozi wetu,” alisema Mwakalebela