×

Mourinho Atua Tottenham, Akabidhiwa Mikoba ya Pochettino

KLABU ya Soka ya Tottenham Hotspur ya Uingereza, imemtangaza Mreno, Jose Mourinho,  kuwa kocha wao mkuu baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu hadi mwishoni mwa msimu wa 2022/2023.

 

Tottenham imefanya uamuzi huo baada ya kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wake, Mauricio Pochettino, aliyedumu kwa miaka mitano na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza.

 

MANENO YA KWANZA YA JM BAADA YA KUWA SPURS MANAGER:

“Nina furaha ya kujiunga na klabu hii yenye historia nzuri na mashabiki wenye moyo na timu yao. Ubora wa kikosi na mfumo wa kukuza vipaji wa klabu hii unanifurahisha sana. Kwenda kufanya kazi na wachezaji ambao wananivutia inanipa hamasa zaidi”

Mourinho anaongeza orodha ya klabu ambazo amewahi kuzifundisha zikiwa ni: FC Porto, Inter Milan, Chelsea, Real Madrid, Manchester United na sasa ni Spurs.

 

Mauricia Pochettino aliwahi kumchapa Jose Mourinho 3-0 kwenye mechi ya ligi kuu ya Uingereza. Ilikuwa ni mwezi Agosti 2018 kwenye mechi ya Spurs dhidi ya Man United ambapo magoli yalifungwa na Harry Kane (moja) na Lucas Moura  mawili.

 

 

Mechi za Mourinho akiiongoza Spurs kabla ya mwaka 2019 haujaisha zitakuwa ni hizi hapa:

23/11 – West Ham vs Spurs (EPL)
26/11 – Spurs vs Olympiakos (UCL)
30/11 – Spurs vs Bournemouth (EPL)
4/12 – Man United vs Spurs (EPL)
7/12 – Spurs Vs Burnley (EPL)
11/12 – Bayern Munich vs Spurs (UCL)
15/12 – Wolves vs Spurs (EPL)
22/12 – Spurs Vs Chelsea (EPL)
26/12 – Spurs vs Brignton and Hove (EPL)
28/12 – Norwich Vs Spurs (EPL).