MSANII mkongwe wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Cheka Hija Mzee, maarufu kwa jina la ‘Bi Cheka’ amefariki dunia mchana huu wa Novemba 28, 2019, akiwa na umri wa miaka 73, katika Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.
Kifo cha msanii huyo mkongwe kimethibitishwa na mtoto wake wa kiume, Adam Juma, ambaye amesema kuwa mama yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.
Familia ya marehemu inaendelea na mipango ya mazishi ambayo itaitangaza.
Bi Cheka atakumbukwa kwa umahiri wake wa ku-rap ambapo aliwahi kufanya kazi nyingi za muziki hasa akiwa na Kundi la TMK. Baadhi ya wasanii aliowahi kufanya nao ngoma ni Mheshimiwa Temba na marehemu Godzilla.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.
Baadhi ya ngoma alizowahi kuimba Bi Cheka ni hizi.