×

Mzee Miaka 102 Mwenye Watoto 60, Wajukuu 70 Afungua Shule

MZEE Meshuku Mapi Mukari almaarufu mzee Laibon, kutoka jamii ya kifugaji, mwenye umri wa miaka 102 na wake wanane, watoto zaidi ya 60 na wajukuu zaidi 70, amesema kuwa licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu nyumbani kwake, wameweza kuishi kwa amani bila migongano yoyote.

Laibon, mkazi wa Kijiji cha Esilalei, wilayani Monduli, mkoani Arusha, anasema kuwa amelazimika kufungua shule ambayo itaweza kuwa mkombozi kwa wajukuu zake na wale watoto wanaoishi jirani na eneo hilo, ambayo imechagiza hamasa ya elimu katika jamii hiyo ya kifugaji, ambayo kwa muda mrefu imekuwa nyuma katika masuala ya elimu.

Mwalimu Abel Langa, ambaye ni mmoja ya walimu katika shule iliyoanzishwa na Laibon, amesema muitikio wa elimu katika jamii hiyo, umeendelea kuwa mkubwa na hii imetoa hamasa kubwa ya elimu kwa jamii hiyo.

Aidha, katika hatua nyingine, familia yake imeanza kufuata na kuabudu imani ya Kikristo na kuachana na baadhi ya mila potofu kama vile ukeketaji na unyanyasaji wa kijinsia.

Leave a Comment