×

Nay na Shamsa Mambo Safi!


BAADA ya penzi lao kufa na kuzikwa, imebainika kwamba, kumbe mwigizaji wa Bongo Muvi, Shamsa Ford na staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ mambo yao ni safi kinoma.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Shamsa amesema, yeye na Nay ni washkaji ileile na wanakutana mara kwa mara kupiga stori.

 

“Kuachana siyo vita. Tumeachana, lakini tumebaki kuwa marafiki, ukitukuta mahali unaweza kusema tumerudiana, yaani ni fulu vicheko na juzikati tu alikuja dukani kwangu kumnunulia madera mama yake, tulicheka sana siku hiyo,” amesema Shamsa.

 

Wawili hao waliwahi kuwa wapenzi kabla Shamsa hajaolewa na mfanyabiashara Chid Mapenzi. Hata hivyo, Shamsa kwa sasa yupo huru, ameshaachana na mumewe huyo, lakini amekuwa akisema wazi kuwa, miongoni mwa wanaume aliowahi kuwa nao, basi Nay alikuwa mtu bomba kinoma.

 

Leave a Comment