STAA wa Bongo Fleva, Ali Kiba au King Kiba amefanya shoo ya kibabe iliyoandika historia na kuacha alama kubwa kwenye Jukwaa la Fiesta usiku wa kuamkia leo, Jumatatu, desemba 9, 2019.
Tamasha hilo ambalo ni kilele chake kimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam limehudhuriwa na amelfu ya mashabiki huku wasanii zaidi ya 38 wakipata fursa ya kupanda jukwaa na na kuwapa burudani mashabiki wao.